Serikali
wilayani Bunda Mkoa wa Mara imefanikiwa
kupiga vita mauaji ya walemavu wa ngozi yaani {Albino} sababu ikitajwa kuwa
Jamii imekuwa na uelewa mkubwa juu ya walemavu hao katika kuwalinda,kuwathamini
pamoja na kuwajali.
Akitoa
Tarifa kwa Vyombo vya Habari Mwenyeketi wa kamati ya ulinzi na usalama wa
wilaya hiyo Joshua Mirumbe alisema hatua hiyo ya kutokuwa na mauaji yeyote ya
Albino kwa mwaka 2014 hadi sasa ni ushirikiano mzuri kati ya kamati ya ulinzi
na usalama pamoja na jamii katika kuhakikisha kuwa dhana potofu katika vichwa
vya watu inatoweka.
Mirumbe
alisema katika wilaya ya Bunda kuna jumla ya walemavu wa ngozi {albino} 65
licha ya kuwa idadi ni dogo lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama
vile ukosefu wa kofia za kukinga miale ya jua ,ukosefu wa mafuta ya kulainisha
ngozi.
Pamoja Na
jitihada zilizofanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwa
kushirikiana na jamii lakini mwenyekiti
wa kamati hiyo alisema jamii iendeleee kuwa balozi kwa wengine katika
kutokomeza suala hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni