Imeelezwa
kwamba Kata ya Namuhula iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani
Mara inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya barara.
Akiongea na
wanahabari Diwani wa Kata hiyo Amon Jogoro ambapo alieleza kuwa uchakavu wa
miundombinu hiyo ulisababishwa na mvua zilizokuwa zikinyesha siku za nyuma.
“Barara zote ambazo
ziko katika Kata yangu ni mbovu na hazipitiki kwa urahisi hasa kwa Magari” Alisema
Jogoro.
Jogoro alisema
yeye kama mwakilishi wa wananchi katika
halmashauri ya wilaya ya Bunda Alisha wasilisha taarifa za uchakavu wa miundo
mbinu hiyo na tayari imeshawekwa kwenye mpango wa kurekebishwa kupitia bajeti
ya mwaka wa Fedha wa 2016/17.
Katika hatua
nyingine Diwani huyo alizungumzia kuhusu tatizo la madawati katika kata yake
ambayo inakabiliwa na upungufu wa Madawati 1300.
“Kata yangu katika
halmashauri ya wilaya ya Bunda inaonekana kuwa na upungufu mkubwa wa madawati
tofauti na kata zingine”Alisema Jogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni