Shirika la PCI International la
nchini Marekani limejenga vyoo 15 na matenki ya kuvunia maji 6 vyote vikiwa na
thamani ya sh.milioni 617.5 kwa shule 15 za msingi za wilayani Bunda.
Mratibu wa shirika hilo wilayani
humo,Bundala Ng’wandu alisema kuwa PCI inafanya hivyo kwa lengo la kuboresha
mazingira ya kujifunzia na kufundishia mashuleni huku likiboresha pia afya za
wanafunzi.
"sisi kama PCI tumeamua kufany hivi ili tuboreshe mazingira ya kujifunzi mwanafunzi"
Mapema mwenyekiti wa kijiji cha
Kisorya cha wilayani humo,Novatus Ibrahimu,akiongea kwa niaba ya serikali za
vijiji zilizokabidhiwa vyoo hivyo alisema hatua hiyo itachangia kuinuka kwa
taaluma mashuleni.
"Jamani PCI tunawashukuru sana maana hatua hii ni zuri na itachangia kuinua kiwango cha taaluma kwa watoto wetu"
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Bunda,Joshua Mirumbe aliyevipokea vyoo hivyo,aliitaka jamii kuvitunza na
kuviendeleza kwa manufaa ya vizazi vijavyo huku akisistizia uwepo wa mahusiano
mema kati ya wafadhili na jamii.
" ni kwamba sasa kazi imebaki kwenu kama jamii vitunzeni vyoo hivi ili na vyenyewe viwatunze mkifanya hivyo mtaendelea kujenga mahusiano mazuri na PCI"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni