Mitaro
iliyopo katika soko la jioni (genge la jioni) katika mji wa Bunda mkoani Mara
imegeuka kuwa sehemu ya kujisaidia haja dogo kwa akina mama wanaouza bogaboga eneo
hilo hali ambayo inaweza kuathiri afya
za watu wanaofika eneo hilo.
Sauti ya
Bunda Blog ilifika eneo hilo na kushundia wakina mama hao wakijisaidia katika
mitaro hiyo huku wakisema wanafanya hivyo kwa kuogopa kuibiwa bidhaa zao kwani
hujisaidia huku macho kwenye bidhaa zao.
“Sisi huwa
tunafanya hivi muda huo macho umetazama mbele kama nyanya zao au samaki na vitu
kama hivyo ili tu mtu asije akachukuwa bila idhini”walisema
Wakina mama
hao licha ya kukili kuwa jambo hilo sio zuri lakini waliilalamikia serikali ya
halmashauri ya mji wa Bunda kwa kushindwa kuweka miundombinu bora katika soko
hilo.
“tunafahamu
kuwa hiki kitu sio kizuri sasa tufanyeje kama halmashauri yetu haitutengenezei
mazingira mazuri ya biashara”walisema
Sauti ya bunda
blog ikamtafuta Mkurugezi wa mji wa Bunda Ally J. Ally ambapo alisema
halmashauri ya mji wa Bunda imejipanga kuboresha mji wake ili kufikia katika
hatua ambayo ni zuri na kwamba na mambo ya kujisaidia hovyo yatakwisha.
“Ni seme tu
kuwa maisha ambayo tuliyazoe kama wana bunda ya kujisaidia hovyo tuyaacha maana
mji wetu sasa unakuwa” alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni