Diwani wa
kata ya Bunda Mjini katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoa Mara Joash Kunaga
ameipongeza Redio Mazingira Fm (sauti ya jamii) iliyopo mjini Bunda kwa kazi
kubwa wanayoifanya ya kuhabarisha jamii kupitia
vipindi vyao vya kila siku hali ambayo imesaidia pa kubwa katika jamii kufahamu
mengi.
Joash
aliyazungumza hayo wakati alipotembelea studi za redio hiyo zilizopo mtaa wa
Bank ya NMB mjini ambapo alisema hana budi kuishukuru redio hiyo kwa kuelimisha
jamii juu ya maswala mbalimbali ya kijamii.
“ni
siwe mchoyo wa sifa kiukweli niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya kwani
inaonyesha matokeo chanya kwa jamii” alisema
Katika hatua
nyingine Diwani huyo aliwataka viongozi pamoja na wafanyakazi wa redio hiyo
waendelee kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuendelea kuwa vizuri katika
uhabarishaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni