Jamii katika halmashauri ya mji wa
Bunda imetakiwa kutunza vyanzo vya maji kwajili ya uhai wa maisha yao na kwa
taifa kwani mazingira yanapoharibika yanaharibu rea ya juu na kusababisha
mabandiliko ya tabia ya nchi hali inayopelekea kukosekana kwa mvua au kuwepo
kwa mvua kupita kiasi.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho
ya usafi wa mazingira Duniani Ambapo mji wa Bunda wakiwa mwenyeji kimkoa Mkuu
wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe alisema jambo la usafi wa mazingira ni la
kila mtu na kwamba watumishi wa serikali waendelee kushirikiana na jamii katika
kuhakikisha mazingira ya mji wa Bunda yanakaa
vizuri.
Mirumbe pia alisema jamii ijenge
tabia ya kupanda miti mara kwa mara ili kuendelee kuweka mazingira katika hali ya
usafi wakati wote.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa
halmashauri ya Mji wa Bunda Masumbuko Majura alisema kuwa katika kuadhimisha
kilele hicho cha usafi wa mazingira wamepanda miti 117 ambayo itasaidia kutunza
chanzo cha maji cha Salanga kilichopo katika kata ya Nyasura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni