Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumnbe amepiga marufuku
uingiaji wa mtu yeyote katika eneo la ufukwe wa ziwa Victoria linalomilikiwa na
kituo cha kulelea watoto yatima cha Bunere Orphanage Centre cha wilayani humo.
Mirumbe amechukua hatua hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa za
kuwepo kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Bunere za kutaka kulivamia eneo hilo
kwa ajili ya kuendeshea shughuli za uvuvi.
"Nisema hivi sitaki kuona au kusikia mtu yeyote anapitapita katika ufukwe huu ambao uko ndani ya eneo hili la kituo hiki na kwamba"alisema Mirumbe
Amesema kwa kuwa watoto walioko katika kituo hicho
kinachomilikiwa na kanisa la Waadventista wa Sabato Konfrensi ya Mara ni wenye
mapungufu mbalimbali wakiwemo albino,ni vema kusiwepo na maingiliano holela
ndani yake.
"Sasa hawa wananchi wanaopita pita hapa pingine twaweza kutowaamini maana hawa watoto waliopo hapa wengine ni walemavu wa ngozi ni seme tu kwamba sitaki kuona hawo watu wakiindelea kuwa wasumbufu"alisema Mirumbe
Awali msimamizi wa kituo hicho,Nashon Malima amesema tangu
kilipoanzishwa mwaka 2009 hadi sasa kinao watoto 117 ambao hupatiwa mahitaji
yote muhimu na Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni