Jumatatu, 13 Juni 2016

TARAFA YA CHAMURIO WILAYA YA BUNDA YAPATA MADAWATI 308 KATIKA HARAMBEE YA UCHANIAJI MADAWATI.



Katika kuhahikikisha kwamba wanafunzi wa shule za msingi na sekondary hawakai chini katika tarafa ya  chamurihu iliyopo wilayani Bunda mkoani Mara wadau wa elimu katika tarafa hiyo wamefanya harambee na kupata jumla ya madawati mia tatu na nane ambapo  Harambee hiyo  imefanyika katika mji mdogo wa nyamuswa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri wa wilaya ya Bunda Isack Mahela  kwa niaba ya mkuu wa wilaya.

Akizunguma na vyombo vya habari Afisa tarafa wa chamurihu Boniphace Maiza alisema licha ya mwitikio kuwa mdogo wa wadau lakini wamefanya kitu kikubwa ambacho walikuwa hawakitarajii kukiona katika harambee hiyo.

 "ni kweli kuwa wadau wamejitokeza kwa asilimia dogo lakini inapaswa kuwashukuru kwa kazi kubwa waliyoifanya licha ya uchache wao"

Afisa tarafa huyo alisema idadi ya madawati wanayo yahitaji bado haijakamilika maana tarafa yao inaupungufu wa madawati 2161 huku akisema bado wanalifanyia kazi ili kufikia june 30 wawe wamekamilisha.

"hatuishii hapa bado tutendelea kushirikisha wadau ili kufikia june 30 tuwe tumemaliza tatizo hili"   

 Hali hii ya tarafa kuanza kufanya harambee za uchangiaji madawati katika wilaya ya bunda ilikuja baada ya wadau wa elimu wa wilayani humo  kupendekeza kuwa kazi hiyo ianzie vijijini ili nao walioko vijijini  washiriki katika suala hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni