Baadhi ya wabunge wameonesha
wasiwasi kuhusu kupunguzwa kwa fungu la fedha katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
wa Hesabu za Serikali na kuonya kuwa huenda hatua hiyo ikapunguza kasi ya
utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Wabunge hao walionesha wasiwasi huo
kwa nyakati tofauti bungeni mjini Dodoma, wakati wakichangia hotuba ya Bajeti
Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2O16/17 inayoanza kutekelezwa Julai mosi,
mwaka huu.
Miongoni mwa wabunge hao ni mbunge
wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), aliyesema kuwa, kupunguza fedha katika ofisi
hiyo ni kumkwamisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kufanya kazi yake kwa ufanisi na tija.
" kupunguza fedha katika ofisi
hiyo ni kumkwamisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kufanya kazi yake kwa ufanisi" alisema kangi
Kwa mujibu wa Kangi, kitendo hicho
kinaweza kutafasriwa kama cha kuukumbatia ufisadi kwa sababu ofisi ya CAG ndio
inayofanya kazi ngumu na kubwa ya kuwafichua mafisadi nchini, hivyo inahitaji
kujitosheleza kibajeti na hivyo kuiepusha na utegemezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni