Pamoja
na hali hiyo, alisema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na
mchana kuhakikisha anaisaidia nchi pamoja na wapigakura wake na kuwa na
maendeleo ya kweli na Jumatano ya Julai 29, ataripoti bungeni.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana baada ya kurejea akitokea nchini Israel ambako alikwenda kwa shughuli zake binafsi.
Alisema
licha ya mtihani uliomkuta, kwa sasa yupo imara kwa ajili ya
kuwatumikia wapigakura wake kwa kuwawakilisha vema ndani ya Bunge.
“Niko
imara kabisa na nina nguvu na matumaini mapya, nimeingia nchini jana
(juzi) nikitokea nchini Israel ambako nilikuwa na shughuli zangu
binafsi. Unajua mimi ni mtaalamu (wa mawasiliano) na wewe unajua kabla
sijaingia kwenye siasa nilikuwa nafanya nini".
“Kifupi
ninasema nilikwenda Israel kwa shughuli zangu binafsi kabisa ambazo kwa
kipindi cha wiki tatu nilizokuwa huko nimefanya. Hata wanaosema
nilikwenda kulia kwa Bwana nao ni mawazo yao, maana unajua ile ni nchi
takatifu kutokana na historia yake,” alisema Kitwanga"
Alipoulizwa
amepokeaje hatua ya kufutwa kwake kazi na Rais John Magufuli kwa kile
kilichoelezwa ni ulevi, alisema kwa sasa hawezi kusemea jambo hilo kwani
aliyemteua ndiye mwenye mamlaka ya kumwajibisha.
“Rais
ni mtu mkubwa anaweza kufanya jambo lolote ili mradi havunji sheria,
hata kilichotokea kwangu ni mamlaka yake halali, ingawa Mungu ndiye
muweza wa kila jambo. Mimi ni Mkristo safi, nasi tumefundishwa kusamehe
saba mara sabini na kusahau yaliyopita,” alisema kitwanga
Akieleza
mikakati yake, Kitwanga alisema kuwa baada ya kuripoti bungeni wiki
ijayo, atakuwa na ziara ya wiki tano ndani ya jimbo lake ambako
atazungumza na wapigakura wake na kueleza yaliyomsibu hatua kwa hatua.
“Sitaki
kuingia ndani sana ila mengine nitayasema nikiwa jimboni, lakini si kwa
lengo la kubishana na mtu, na uzuri kila hatua ambayo nimepitia hata
wapigakura wangu walikuwepo kwa uwakilishi wa madiwani wa Misungwi ambao
walikuwa mjini Dodoma,” alisema kitwanga
Mei
21, mwaka huu, Rais Magufuli alimng’oa Kitwanga kuhudumu kama Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na madai ya ulevi, huku taarifa zaidi
za ndani zikieleza kuwa alianza kushughulikiwa bila yeye mwenyewe kujua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni