Baadhi ya Madiwani
katika halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara waliitaka idara ya kilimo ya
halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria mawakala wa pembejeo ambao
wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kubabaisha.
Wakiongea kwenye kikao
cha baraza la halmashauri hiyo madiwani hao walisema baadhi ya mawakala hao
wamekuwa wakitoa taarifa za utendaji kazi wao tofauti na hali halisi
ilivyo jambo linalo changia kuzorota kwa
uzalishaji wa mazao ya kilimo wilayani humo.
Mmoja wa madiwani hao
mramba Simba Nyamkinda wa kata ya ketare alisema katika kudhibiti hali hiyo
halmashauri haina budi kuweka mfumo maalumu wa kufuatilia nyendo za mawakala
hao ili wale watakao bainika kuwa wababaishaji waadhibiwe kisheria.
Hata hivyo afisa
kilimo wa halmashauri hiyo Serapion Rujuguru licha ya kukili kuwepo kwa mawakala wasio waaminifu ambao
halmashauri imewaadhibu kisheria lakini pia aliwataka madiwani kusaidia
kuwadhibiti mawakala hao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni