Serikali
katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda Mkoani Mara imeombwa kuwatazama kwa jicho
la huruma vijana wa Scouti katika kuwawezesha chakula pamoja na vifaa vya
kutumia wakati wakiwa kambini vifaa hivyo ni kama vile Mahema na Masufulia ya
kupikia chakula hali itakayo saidia vijana kutimiza wajibu wao bila shida
yeyote.
Akizungumza na
blog hii Kamishina Msaidizi wa scouti wilaya ya Bunda Chabwene John Musimo alisema
kama vijana wanapata mahitaji muhimu wakiwa kambini ni kweli kuwa watendelea
kupenda scouti bila kuwa wasumbufu.
“serikali
yetu ya wilaya ya bunda itutazame kwa jicho la huruma ili tuweze kufikia
malengo yetu kama scouti”
Chabwene
alisema kuwa scouti inafundisha jinsi ya kuishi na watu katika mazingira yeyote
na kwamba inasaidia vijana wengi
kujiepusha kuingia katika vikundi vya matendo maovu kama vile vibaka mtaani.
“scouti kama
scouti inasaidia mambo mengi sana inapunguza vibaka mtaani kupitia vijana ambao
tunawapa mafunzo ya jinsi ya kuishi na watu katika mazingira yeyote ndio hao
wanakuwa mabalozi wema katika jamii”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni