Katibu wa Chama
cha mapinduzi ccm mkoa wa Mara amewataka wananachama wa chama hicho wanaovujisha siri za vikao vya chama kabla ya kufanyiwa
kazi wachukuliwe hatua maana wataendelea
kukitia dowa chama hicho.
Akizungumza
katika kikao mara baada ya kutembela miradi mbalimbali ya maendeleo jamii
katika kata ya ketare wilayani Bunda mkoani mara katibu Adamu Ngalawa alisema
kwamba majina yao yaorodheshwe na ya pelekwe kwa katibu wa chama wa kata na
wajadiliwe ili wapewe barua ya onyo.
“ Ni seme tu kwamba kwa hawa wanachama wanaotusaliti kwa
kuvujisha siri ya vikao vyetu kabla utekelezaji basi majina yao yaorodheshwe
mara moja na yapelekwe kwa katibu wa chama wa kata”
Licha ya hivyo
alisisitiza kwamba viongozi hao endapo watapewa barua ya onyo na
wasibadilike basi wachukuliwe maamuzi ya kufutwa uanachama .
“Lakini pia baada ya kuorodhesha majina yao wanatakiwa wapewe
onyo na wasipo badilika hatuna budi kuwapa mkono kuwa hatuwataki kwenye chama maana
wamepoteza sifa ya kuitwa wanachama wa ccm”
Kwa upande
wake diwani wa kata ya Salama kupitia
chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Merchard Ikungura alionyeshwa kutoridhishwa na mwenendo wa
kikao hicho kwa kile alicho dai kuwa alitegemea kuona tathimini ya utekelezaji wa ilani ya chama cha
mapinduzi na badala yake wamezungumzia
suala la kujipanga kichama katika uchaguzi ujao wa chama.
“Nami nisema kuwa sijaridhishwa na hiki kilichofanywa na hawa
wenzetu wa ccm mimi nimefika hapa nikitarajia kuwa tunajadili utekelezaji wa
ilani kumbe ndivyo sivyo kabisa na vile nilivyokuwa nafahamu”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni