Wakizungumza katika kijiji cha Kwedichocho baadhi ya viongozi wa
serikali ya kijiji na wakazi wake walisema hatua hiyo imekuja baada ya
baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mazingara kumuuzia mwekezaji hekari
zaidi ya 400 zenye makazi ya watu zaidi ya 1000 pamoja na shule hatua
ambayo wanafunzi wameanza kutishiwa kuondoka kwa sababu mwekezaji
anataka kulifanyia kazi eneo la ardhi ikiwa ni pamoja na majengo ya
shule pamoja na nyumba ya mwalimu.
"siku hizi watoto wetu wanatishiwa kuondoshwa katika eneo hili la shule kitu ambacho ni kigumu sana"walisema wananchi"
Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho Saleh Sadick
alisema wakazi wa vitongoji vya Kwedichocho na Mkulumilo vyote vilivyopo
katika kata ya Mkata hawatakubali kuondoka katika eneo hilo linalodaiwa
kuwa ni eneo la kijiji cha Mazingara hatua ambayo inaweza kusababisha
uvunjifu wa amani baina ya pande hizo mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni