Jumatano, 8 Juni 2016

WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI PIKIPIKI WATAKIWA KUFAUTA SHERIA ZA KUMILIKI VYOMBO HIVYO.



Wamiliki wa vyombo vya moto hususani pikipiki wametakiwa kuajiri madereva wenye sifa na  wanao tambulika kisheria ili kuepusha ajali  zinazo jitokeza mara kwa mara.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Trafiki wilaya ya Bunda Rose John Mbaga wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na swala zima la usalama barabarani ambapo alisema kuwa ajali nyingi zinazo tokea mara nyingi zimekua zikisababishwa  na madereva  wasio na sifa wanao ajiriwa na wamiliki wa pikipiki.

"Nivema wamiliki wa vyombo hivi wakaajiri madereva walio enda  kupata elimu na leseni inayo ruhusu kutumia vyombo vya moto" Alisema Mbaga

Mbaga alisema wamiliki hao wamekuwa wagumu kutii wito pindi wanapo itwa kupewa ufafanuzi au elimu  kuhusu  watu wanao takiwa kuajiriwa kwa kazi hiyo na wenye sifa na wanao tambulika  kisheria.

Tumekua tukipata  shida sana tunapo jaribu kuita wamliki wa vyombo hivyo kuwapatia elimu kwa sababu wengi wao hawahudhurii hivyo inatuwia ugumu kutoa elimu hiyo kwa watu kama hawa. alisema Mbaga 

Mbaga aliongeza kwa kusema  kwamba kwa mmiliki yeyote atakaye toa chombo chake kwa dereva asiye na leseni wote wawili watachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yao ili liwe fundisho kwa wengine watako kwenda kinyume na  sheria.

Hata  hivyo Mbaga alitoa onyo  kwa madereva na abiria kuacha kubeba abiria zaidi ya mmoja kwani wakigundulika sheria itachukuwa mkondo wake na kupigwa faini ya sh 30000 kila mmoja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni