Chama cha
Walimu (CWT) wilayani Bunda katika mkoa wa Mara kilieelezea kupokea kwa
masikitiko makubwa ugonjwa wa mwanachama wake ,mwalimu Joyce Maugo anayedaiwa
kuathirika kiakili.
Katibu wa
CWT wilayani humo Kambula Maraba
aliwaambia waandishi wa habari kuwa
ugonjwa wa mwalimu huyo umekiweka chama
hicho katika hali tofauti kwani bado kinampigania ili arejeshwe katika utumishi.
“Chama
chetu kinasikitika sana kwa ugonjwa ulio mkumba mwanchama wetu japo tunafanya
jitihada za kumrejesha katika hali yake ya kawaida” alisema Kambula
Alisema
ingawa haijafahamika chanzo cha mwalimu huyo kupatwa na ugonjwa huo lakini
huenda ukawa ulishababishwa na hatua ya mwajiri kumwondoa kwenye orodha ya
watumishi kwa kudai kwamba ni mtumishi hewa.
Hata hivyo
Kambula alisema CWT wilayani humo ilianza mara moja mchakato wa kuhakikisha
kwamba anarejeshewa utumishi wake pindi
tu pindi tu ilipopokea taarifa kufutwa na kwamba kwa sasa inamwombea apone
haraka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni