Eneo la Unga Limited, jijini Arusha
Mtoto
wa miaka minne amenajisiwa na kuvunjwa shingo na kutupwa kandokando ya
njia ya watembea kwa miguu karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50
kutoka nyumbani kwao jijini Arusha.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Yusuf Ilembo, tukio la kunajisiwa kwa mtoto huyo wa kike
lilitokea Juni 20, mwaka huu saa 3.30 usiku kwenye makaburi ya baniani
Kata ya Unga Limited.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Ilembo alidai mtoto huyo ambaye kwa sasa ni marehemu
alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika saa
12 jioni kwa mujibu wa marafiki zake (majina yamehifadhiwa) wanasema
alifika mtu mmoja mwanamume mrefu.
Kwa
mujibu wa watoto hao, mwanamume huyo alikuwa amevaa suruali na
kumwambia mtoto huyo amfuate akamnunulie pipi na hapo ndipo alipomfuata
huyo mwanamume huyo na hakurudi tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni