Jumamosi, 18 Juni 2016

MIRUMBE KULA SAHANI MOJA NA VIBAKA MTAANI.





Mkuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara Joshua Mirumbe amewataka viongozi wa serikali ngazi za vijiji na kata kuhakikisha kwamba wanakomesha vitendo vya uhalifu katika maeneo yao ili hali ya amani na utulivu iimarike.

Mirumbe alisema ameamua kutoa agizo hilo baada ya kubainika kuwepo kwa vitendo vya uhalifu katika baadhi ya maeneo wilayani humo vinavyowafanya watu waishi katika hali ya wasiwasi.

“Nimeamua kutoa agizo hili baada ya mimi kubaini kuwa kuna vitendo vya uhalifu vinatendeka katika maeneo baadhi ya wilaya hii  sasa  kwa wewe kiongozi wa serikali  ya kijiji na kata hakikisha unakomesha vitendo hivyo”

Alivitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kuwepo  kwa kundi la watu wanaowavamia wavuvi wanaofanya kazi zao ndani ya ziwa Victoria na kuwapora zana zao na samaki pamoja na uwepo wa vibaka katika maeneo ya miji wanaowakaba watu na kuwapora mali zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni