Mkuu wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo amesikitishwa na taarifa ya
kwamba wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali ya Manyamanyama wilayani Bunda
wakiwemo wanawake wajawazito na watoto,hujinunulia vifaatiba na dawa.
Kutokana na hali hiyo,Mulongo aliyefika hospitalini hapo kwa
kushtukiza,alieuagiza uongozi wa halmashauri ya Mji wa Bunda kulimaliza mara
moja tatizo hilo huku akiutaka pia kutoa maelezo ya kina kuhusiana na kuruhusu
jambo hilo kutendeka.
Kauli ya mkuu huyo wa mkoa ilikuja baada ya wagonjwa waliolazwa
hospiralini hapo wakiwamo wanawake wajawazito kumweleza kuwa wamekuwa
wakijinunulia vifaa tiba zikiwamo kadi za kliniki na glovu pamoja na kulipia
gharama za matibabu.
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri hiyo,Nicodemus
Masosota aliyeahidi kulishughulikia tatizo hilo haraka iwezekanavyo, alimweleza
mkuu huyo wa mkoa kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa
dawa na vifaatiba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni