Kiongozi
mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe asubuhi ya leo June 13
2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia
kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti.
Pia
alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa
utaratibu wa wito.
Leo jioni Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya dakika 90 .
Baada
ya kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa
chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo
kituoni hapo.
"Wamechukua
maelezo ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa
jana.Baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa
rasmi juu ya nini kitafuta baada ya hapa." Amesema Mwakibolwa
"Kama
alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho
tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja,
wanachama watulie tunaendelea na majadiliano na polisi ili tuendelee na
kazi zetu za kisiasa kama kawaida" Amesema Zitto Kabwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni