Serikali imewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, kuhakikisha
wana wakamata watu ambao wana jihusisha na kuhujumu miundombinu ya
barabara za lami kwa kuchimba na kuiba kokoto, huku wakijua kuwa
barabara hizo zimejengwa kwa gharama kubwa kwa lengo la kuwa saidia
wananchi kuji letea maendeleo.
Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika halmashauri
ya Itigi baada ya waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhe Profesa
Makame Mbarawa kukagua barabara ya Manyoni, Itigi hadi Chaya inayo
jengwa kwa kiwango cha lami, alisema kitendo cha kuchimba barabara na
kuiba kokoto ni jambo ambalo la ajabu na haliwezi kuvumilika, kutokana
na hali hiyo lazima walio husika wakamatwe.
Katika hatua nyingine Mhe Profesa Makame Mbarawa aliwahakikishi
wananchi wa halmashauri ya Itigi kuboresha miundo mbinu ya reli na
mawasiliano ili iweze kutoa huduma nzuri na zinazo endana na wakati.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Manyoni,
Itigi hadi Chaya yenye urefu wa kilomita themanini na tisa point saba
inayo jengwa na kampuni ya Mezaz Syonohadro Cop. Ltd kutoka China meneja
wa Tanroads mkoani Singida mwandisi Leornard Kapongo alisema mradi
umegarimu zaidi ya shilingi bilioni miamoja na tisa fedha kutoka Tanzani
kwa asilimia miamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni