Mheshimiwa
diwani wa kata ya Namuhula katika Halmashauri ya Bunda Amon Jogoro akanusha tuhuma ya mradi wa maji
katika kijiji cha karukekere kuwa hausiki hata mara moja juu ya sakata hilo.
Akiongelea
tuhuma hiyo Jogoro alisema kuwa alisikitishwa na kitendo kilicho tokea tarehe
12 mwenzi wa 5 kwake yeye kupelekwa mahabusu baada ya mkuu wa mkoa wa Mara
Magesa Mulongo baada ya kutoa amri ya
kukamatwa mara moja ili afanyiwe uchunguzi zidi ya sakata hilo.
“Nilisikitishwa
sana na kitendo cha mkuu wa mkoa kuamuru polisi kunikamata wakati mimi ndiye
ninaye pigania sakata hilo maana mimi sijahusika kula hata shilingi moja ya
mradi huo”
Jogoro
alisema mradi huo ulianza mwaka 2010 wakati uo yeye akiwa mwenyekiti wa kijiji
cha karukekere ambapo wananchi walikuwa wanachangishwa fedha na kamati iliyokuwa imeundwa kwajili ya
kusimamia mradi na baada ya ukaguzi uliofanyika mwaka 2014 na mkaguzi wa ndani
kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda alibaini kuwepo kwa shilingi laki tatu
tisini na tisa elfu na mia sita.
Jogoro
alisema kufatia tuhuma hiyo hivyo basi polisi bado wanaendelea na uchuguzi na
wale watakao bainika hatua za kisheria zichukuliwe zidi yao huku ikisisistiza
kuwa yeye hausiki katika tuhuma hiyo.
Sambamba na
hilo Jogoro alielezea suala la usambazaji wa pembejeo za kilimo unaofanywa na
Mawakala ambapo alisema kuwa katika kata yake yenye vijiji vinne ilikadiliwa
kuwa na wanufaika mia nane (800) wa pemejeo hizo lakini hadi sasa walio onekana
kunufaika na pembejeo hizo ni 270 japo kuwa hawakunufaika kama ilivyo kuwa
imekusudiwa.
Aidha alisema
kuwa pembejeo hizo ilikadiliwa kama ifuatavyo:-
Hekali moja
ya shamba la Mahindi ni kg.10,Mifuko miwili ya mbolea ya kupandia na kukuzia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni