Baada ya
Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa Chama Cha
ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12 2016 kwa
lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017.
Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe
kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake
sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower)
kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi
mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi
aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na
hivyo asiwafungulie ukumbi huo.
Hivyo
kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa sana na
hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za
uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni