Mkuu wa wilaya Kahama Vitta Kawawa
amewaagiza maofisa watumishi katika halmashauri tatu zinazounda wilaya hiyo
kubandika majina ya watumishi watakaolipwa mishahara kila mwisho wa mwezi na
watumishi kuhakiki majina yao na watakapobaini majina ya watumishi ambao hawapo
kazini watoe taarifa mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe.
“Tukifanya
hivi tutakuwa tumepiga hatua zaidi yakutusaidia kubaini mapema wafanyakazi hewa”
alisema
Mfumo
huo mpya unaolenga kuendelea kubaini watumishi hewa ulitangazwa na Mkuu wa
wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa wakati akipokea miradi ya maendeleo ya elimu
kutoka katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya Acacia
miradi iliyotekelezwa kwa thamani zaidi ya shilingi milioni 279.
Akikabidhi miradi hiyo ambayo ni
madawati,nyumba za walimu,vyoo vya wanafunzi,pikipiki na majengo ya shule ya
sekondari Bugarama yaliyokarabatiwa,Kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Bw.Benedict Busunzu,alisema kampuni ya Acacia imejikita katika
kusaidia sekta ya elimu ili kuiwezesha serikali kuzalisha wataalamu,watakaoliwezesha
taifa kuingia katika soko la ushindani wa ajira duniani.
“ kampuni
ya Acacia imejikita katika kusaidia sekta ya elimu ili kuiwezesha serikali
kuzalisha wataalamu” alisema
Baadhi
ya waalimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo walidai kuwa
kumekuwepo na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambao nao walijitokeza kuhakikiwa
ambapo zoezi la kubandika majina ya watumishi litasaidia kuwabaini.
kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa baada ya zoezi la uhakiki wa wafanyakazi katika
wilaya ya kahama,inasemekana shilingi milioni 360 ambazo zingeweza
kutatua kero mbalimbali za wananchi zimetumika kulipa wafanyakazi hewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni