Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna msaidizi mwandamizi wa
polisi Ahmed Msangi,amesema tukio hilo limetokea Mei 31 majira ya saa
4.10 usiku,baada ya askari polisi waliokuwa doria katika maeneo hayo
kuwatilia shaka watu watatu waliokuwa wakipita katika barabara iliyopo
kati ya kituo cha Radio Free Afrika na kiwanda cha Mwanza Fishing ambao
walikuwa wamebeba begi na askari walipowapa amri ya kusimama ili waweze
kuhojiwa pamoja na kupekuliwa hawakutii amri hiyo.
Hata hivyo baada ya jambazi huyo kuuawa,askari walikagua bunduki na
kubaini kuwa namba za bunduki hiyo aina ya Short machine gun,( SMG )
zilikuwa zimefutika na risasi 16 zilikutwa ndani ya magazini,huku begi
likiwa na jaketi kubwa hali iliyoashiria kwamba watu hao walikuwa
wamejipanga kwenda kufanya uhalifu mahali kwingine,mwili wa marehemu upo
katika hospitali ya rufaa Bugando kwa utambuzi ambapo upelelezi na
msako wa kuwakamata waliokimbia bado unaendelea.
Katika tukio jingine,mwanafunzi wa Chuo cha mipango ya maendeleo
vijijini Kanda ya Ziwa kituo cha Mwanza Frank Chambi anashikiliwa na
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mkazi wa Bwiru
Dotto Japhet aliyeuawa kwa kupigwa na jiwe kichwani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni