Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda
ya ziwa imefanya msako mkali katika maduka ya dawa, maduka ya vipodozi
na maduka ya vyakula katika maeneo tofauti wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na kukamata
shehena ya bidhaa mbalimbali ambazo hazifai kutumika kwa matumizi ya
binadamu.
Akizungumzia sakata hilo mkaguzi wa dawa kutoka mamlaka ya chakula
na dawa kanda ya ziwa, Bw.Andrew Mwabuki amewatahadharisha
wafanyabiashara wa dawa wilayani Kahama kuzingatia vigezo na masharti ya
biashara hiyo, huku akizitaja takwimu za bidhaa ambazo zimekamatwa na
kuteketezwa.
Makaya William Msonda, akizungumza kwa niaba ya mkaguzi mkuu wa
mamlaka ya chakula na dawa ofisi ya kanda ya ziwa amesema ili bidahaa
kutoka nje ziruhusiwe kuingia nchini, ni lazima vigezo vilivyowekwa
kitaifa na kimataifa vizingatiwe, huku mfamasia mkuu wa mkoa wa
Shinyanga, Bw.John Mfutakamba akitanabaisha bayana baadhi ya sababu
zinazosababiusha kuwepo kwa bidhaa bandia na vyakula visivyofaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni