Aliyekuwa
Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Mhe.Edward Lowasa ameikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa ilikuwa na dosari nyingi na
imetengenezwa katika mazingira ya kukifurahisha chama tawala.
Mhe.Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani alisema Ripoti hiyo
ya Jumuiya ya ulaya ilitakiwa iende mbele zaidi na kuelezea kile
kilichofanyika nchini kama kilikuwa ni huru na haki kwa mustakabali wa
Demokrasia nchini ambapo pia ameikosoa vikali Tume ya Uchaguzi.
"Na amini mimi ni lishinda lakini niliamua kukaa kimya kwa mustakabali wanchi"
Katika hotuba yake kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani ambao ni wanachama wa CHADEMA ,Mhe.Lowasa alisema
na kila ushahidi kuwa alishinda Uchaguzi Mkuu katika kiti cha urais
mwaka jana lakini ameamua kuwa kimya juu ya hilo kwa mustakabali wanchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni