Sakata
la wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu
Spika, Dk Tulia Ackson limefika pabaya baada ya baadhi ya wawakilishi
hao kuanza kutowasalimia baadhi ya wabunge wa CCM.
Hatua
hiyo ilikuwa dhahiri jana baada ya Ukawa kutangaza kuwa
hawatashirikiana na wabunge wenzao wa chama tawala katika shughuli za
kawaida za kijamii, kama vile michezo na kutumia kantini ya Bunge,
wakisema wenzao wameanza kuwabagua.
Mbali
na kitendo hicho, wabunge hao pia walitoka kimyakimya bungeni baada ya
Dk Tulia kuingia, lakini safari hii hawakufanya mbwembwe za kujiziba
midomo kama walivyofanya juzi.
Jana asubuhi, mbunge
wa CCM Kangi Lugola alisema kuwa alisikitishwa baada ya kudai kuwa
Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu), Lucy Magereli hakumjibu salamu yake
wakati akiingia bungeni licha ya kumsalimia mara tatu na kuwa katika
umbali mfupi wa kusikika.
“Kusalimia
ni jambo la utamaduni wetu. Nilikuwa namsalimia mbunge wa kike wa
Ukawa, lakini hakujibu. Lakini, nikajua ni sababu ya wao kufunga mdomo
na plasta, nikamtania au kwa sababu ya plasta hujibu ili isije kudondoka
hakuitikia,” alisema Lugola.
Alisema
ameshtushwa na hali ilipofikia na hajui sababu za msingi za wabunge wa
Ukawa kufanya vitendo hivyo, kinyume na udugu na utamaduni wa
Watanzania.
Mbunge huyo machachari, alisema Kubenea alimziba mdomo Msigwa kwa mkono ili asizungumze chochote.
Naye mbunge wa Sumve (CCM ) Richard Ndassa alisema jambo wanalolifanya wabunge wa Ukawa siyo jema na halina tija kufanywa na wawakilishi hao wa wananchi.
“Sisi ni wabunge, hivi inapofikia kususa kuongea na wabunge wenzako, hatima yake nini?” alisema.
“Mimi
nilienda kuwasalimia kama kawaida ambavyo huwa tunafanya kwa wabunge
awe CUF, CCM au Chadema, sasa unavyosusa una maanisha nini,” alilalamika Ndassa.
Alisema
kitendo cha kutosalimia ni cha juu sana na kwamba iwapo Ukawa
wanashauriwa na mtu basi inawapasa kuchuja mambo mengine, likiwamo hilo
la kuwasusa wabunge wenzao.
Juzi
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia wakati anawaongoza wabunge
wa Ukawa kutoka bungeni aliwatuhumu wabunge wenzao wa CCM kuwa wanawabagua
Naye Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea alisema; “Leo
tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo
tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa
tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.
“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”
“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni