Jumanne, 7 Juni 2016

KATIBU WA MBUNGE JIMBO LA BUNDA MJINI KAUNYA YOHANA AWATOA WASIWASI WANANCHI WA JIMBO HILO KUHUSU MBUNGE WAO.




Katibu wa Mbunge wa jimbo  la Bunda mjini Kaunya Yohana amelezea kusikitishwa na hatua ya Mbunge wake Ester Amos Bulaya  kusimamishwa kwenye vikao vya bunge vinavyo endelea mjini Dodoma.
Akiongea na wandishi wa habari Kaunya alisema kuwa Mh. Bulaya alisimamishwa kundelea na vikao vya Bunge vinavyo endelea mjini Dodoma ni kwa sababu alikuwa akitetea hoja ya kurushwa kwa matangazo ya vikao vya bunge vinavyo endelea mjini  humo , wananchi  na Taifa kwa ujumla.
  
Pia Kaunya alielezea hatua ambazo zimechukuliwa na viongozi wa upinzani kutokana na hali hiyo ya kusimamishwa kwa wa Bunge wa upinzani ambao ni Ester Bulaya, Tundu Lisu Zito Kabwe, Halma Mdee na wengine watatu na kusema kuwa wameamua kuitisha mikutano ya hadhara katika majimbo yao kwa lengo la kuwaeleza wananchi kwa kinaga ubaga kuhusu jambo hilo la kuzuiliwa kuingia ukumbini na alisema kwamba mkutano huo katika jimbo la bunda mjini utafanyika tarehe 13.6.2016 katika viwanja vya stendi ya zamani.
“Ninawasihi wananchi kuwa wavumilivu kwa hatua iliyo chukuliwa  dhidi ya Bunge wetu na ninawaomba tarehe 13.6.2016 mhudhurie kwa wingi  kwenye mkutano wa hadhara “
Aidha Kaunya alitumia nafasi hiyo kuwatoa wasiwasi washabiki  na wachezaji wanao shiriki katika mchezo wa mpira wa miguu wa  ESTER CUP unao tarajiwa kuanza hivi karibuni kuwa  utakuwepo  kama kawaida licha  ya Mh Mbunge kusimamishwa bungeni kuhudhuria vikao hivyo vinayoendelea mjini humo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni