Viongozi watatu wa Serikali za vijiji katika kata ya murangi katika
Halmashauri ya Musoma vijijini Mkoani Mara wakiwemo wajumbe 25 wa
Serikali za vijiji wamekatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za
ubadhirifu wa fedha mbalimbali za michango ya wananchi.
Agizo la kukamatwa kwa viongozi hao,limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Mara Bw Magesa Mulongo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika
katika kijiji cha Murangi ukijumuisha wananchi wa vijiji vya kata ya
Murangi na Msanja.
Wakizungumza katika mkutano huo mbele ya mkuu huyo wa mkoa wa
Mara,baadhi ya wananchi wamedai kuwa licha ya kuchangishwa kila
kukicha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Maabara na miradi mingine ya
maendeleo katika kijiji hicho lakini viongozi hao wameshindwa
kuwasomea mapato na matumizi huku baadhi yao wakigawana fedha hizo na
hivyo kusababisha ujenzi wa maabara kusimama ukiwemo ujenzi wa choo
katika moja ya shule za msingi kijijini hapo.
Kufuatia kilio hicho cha wananchi,mkuu huyo wa mkoa wa Mara amegiza
jeshi la polisi kuwakamata viongozi maafisa wawili watendaji wawili
wa kijiji na mwenyekiti wa serikali ya kijiji wakiwemo wajumbe wa
serikali na kwamba licha ya kutakiwa kurejesha fedha hizo lakini pia
uongozi wa halmashauri umeagiza kuchukua hatua kali kwa viongozi hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni