Wabunge Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wameijia juu serikali wakipinga mpango wake wa kutaka
kukata kodi, kiinua mgongo chao ambapo walisema kufanya hivyo ni
kuwaumiza bila ya sababu ya msingi na kama italazimika kukatwa kwa
kodi hiyo basi ikatwe kwa makundi ya watu wote ambao waliokuwa
wanapata msamaha huo wakiwemo mawaziri na viongozi wengine
wakubwa wa kisiasa wakisiasa.
Wakichangia hotuba ya bajetia Mh.Hilary Aeishi mbunge wa
Sumbawanga mjini alisema wazo lililoletwa na serikali ni kama
kuwagombanisha na wananchi kwamba wao hawalipi kodi.
Naye Mh.Mbaraka Dau mbunge wa Mafia alisema bajeti ya sasa
inapaswa kuongeza wigo katika vyanzo vipya vya mapato hasa katika
sekta ya utalii na pia serikali imejipambanua vyema katika
kushirikisha sekta binafsi katika kuwaletea wananchi maendeleo
.
Mh.Selemani Zed ni mbunge wa Bukene alitahadharisha serikali
kuhusu mpango wa serikali wa kuelekeza fedha zote mfuko mkuu wa
serikali kisha zirudi kwa halmashauri au taasisi huska ni jambo jema
ila wahakishe kuwa fedha hizo zinarudi katika halmashauri kwa muda
la sivyo halmashauri zingine zinaweza kushindwa kujiendeleza.
Mh.Mwanne Ismail ni mbunge wa viti maalum kutoka Tabora na Mh
George Lubeleje mbunge wa Mpwapwa walitumia muda huo kutaka bajeti
katika sekta ya afya kuboreshwa zaidi kiasi cha fedha kilichotengwa
hakiendani na mahitaji halisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni