Jumapili, 5 Juni 2016

POLISI MWANZA WAFANIKIWA KUUA MAJAMBAZI.

Baada ya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya M-pesa, Tigo pesa, na Airtel Money kushamiri jijini Mwanza, June 5 2016 Jeshi la Polisi Mkoani hapo wamefanikiwa kuwaua Majambazi watatu katika majibizano ya risasi katika mapango ya Mlima wa Utemi Wilayani Nyamagana
May 3 2016 Askari Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama walifanikiwa kumkamata Omary Francis Miaka 28′ mfanyabiashara wa ya nyama ya g;ombe buchani na mkazi wa nyegezi Kijiweni baada ya kupewa taarifa  na raia mwema kuwa mtu huyo anahusika na matukio ya unyang’anyi kwa kutumia silaha, hata hivyo Omary Francis alikiri kuhusika katika matukio hayo.

June 4 mtuhumiwa Omary Francis alikubali kuwapeleka na kuwaonyesha Jeshi la Polisi maficho ya wenzake kwenye mapango ya Mlima wa Utemi.
Kama mnavyofahamu Polisi tumekuwa katika Operation yakuweza kuwasaka Majambazi wanaosumbua mji wa Mwanza, na wengi tumewakata na tulivyowakamata tumeweza kuwauliza nisehemu gani walipo wenzao"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni