Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa
imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa
walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio
la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa
ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.
1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
Kwa
utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka
husika kwa hiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo.
Mikataba
inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingatia
masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidhamu na kufuata sheria na taratibu
za vyuo na mamlaka halali.
Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.
Bodi
ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia
masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa
mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni
kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili
kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Ijumaa, Oktoba 7, 2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni