Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa
ya Uingereza Danny Rose amesema Alan Shearer alikuwa sahihi kuita timu
hiyo ya taifa kuwa inatapatapa baada ya kujiuzulu kwa meneja Sam
Allardyce.
''Nilimtumia ujumbe nikimshukuru kwa kunijumuisha katika kikosi chake, na kunifanya kuwa na heshima ningine katika ulingo wa soka la kimataifa, nikamwambia pole sana kwa kupoteza nafasi yake na kumtakia kila la kheri mbeleni'' alisema Rose.
Allardyce ameingia katika historia ya kukaa kwa muda mfupi katika timu hiyo kwa siku 67 tu, aliingia baada ya Roy Hodgson kubwaga manyanga alipotolewa mapema katika michuano ya Euro 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni