Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Dampo la stendi mpya ya Bunda Mjini lawa kero kwa wasafiri.



Baadhi ya wafanyabiashara wanaofanyia kazi zao katika eneo la stendi mpya ya mabasi  katika halmashauri ya mji wa Bunda wamelalamikia uwepo wa dampo katika stendi hiyo linalotoa harufu mbaya hali inayohatarisha afya zao pamoja na wateja wao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na sauti ya Bunda wafanyabiashara hao walisema kuwa takataka zinazotupwa katika dampo hilo huchukua muda mrefu kuondolewa na mamlaka husika hivyo kuleta kero kwa wateja wao.
“Tuna shida hapa takataka zinazotupwa katika dampo hili lakini  huchukua muda mrefu kuondolewa hapa” walisema

Nao baadhi ya wasafiri na wateja wanaonunua vyakula katika stendi hiyo, waliziomba mamlaka husika kushughulikia tatizo hilo la dampo ili kuepusha magonjwa ya milipuko hasa katika kipindi hiki cha mvua.
“Sisi kama wasafiri tunaomba tu mamlaka husika hili Dampo liondolewe kwani hali itakuwa mbaya kwetu” walisema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni