Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Joseph Kabila Kabange,
amewasili hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara rasmi ya
kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Pamoja
na Rais Magufuli viongozi wengine waliompokea Rais Joseph Kabila
Kabange ni Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi mbalimbali wa Serikali, Mabalozi
na wananchi.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Rais Joseph Kabila Kabange alipokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na
kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye
kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni