Tundu
Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana alishindwa kufika katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku
mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia
kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza.
Lissu
ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa
wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la
MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa
kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.
Mdhamini
wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake
mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Ibrahim
alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu
yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi
akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi
hiyo.
“Lissu ni wakili pekee wa mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema Kibatala.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.
Katika
kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa kufuatia kunukuliwa
akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la MAWIO ikiwa
na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni