Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte
amerejelea tena shutuma zake dhidi ya Rais Obama na viongozi wengine wa
nchi za Magharibi wanaopinga mpango wake wa kupambana na walanguzi wa
dawa za kulevya.
Kiongozi huyo amesema Bw Obama anaweza "kwenda jehanamu".Umoja wa Ulaya, ambao pia umemkosoa Bw Duterte, unaweza "kuchagua kwenda eneo la kutakasia dhambi ndogo, kwa sababu jehanamu kumejaa", amesema.
Watu karibu 3,000 wameuawa tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mwezi Juni.
Watu wanaoshukiwa kulangua mihadarati au kuwa waraibu wa dawa hizo wamekuwa wakiuawa na maafisa wa polisi na magenge yanayoungwa mkono na serikali.
Bw Duterte amesema Urusi na China wako tayari kuwa washirika wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni