Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila ametupilia
mbali shutuma kwamba amesogeza mbele tarehe ya uchaguzi ili aendelee
kung'ang'ania madarakani.
Rais Kabilla amewaambia waandishi wa
habari jijini,Dar es salaam kuwa lengo kuu la Serikali yake kubadili
ratiba ya uchaguzi ni kutokuwa na maandalizi ya kutosha.
Amesema
serikali yake isingependa kuacha idadi kubwa ya wananchi wake na wengi
wao wakiwa ni vijana ambao hawakujiandikisha kupiga kura na wakose haki
yao ya kupiga kura .
Mwishoni mwa wiki iliyopita,kiongozi wa tume
ya uchaguzi nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo alitangaza
uwezekano wa kusogezwa tarehe ya kupiga kura hadi hapo desemba 2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni