Kwa
kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana nchini, benki ya NMB imedhamini
vijana watano kutoka nchini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya
mashua ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Luanda, Angola kuanzia Oktoba 6
- 13, mwaka huu.Akizungumzia udhamini huo wa Milioni 10 na jezi kwa
vijana hao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema NMB kama benki ya
kitanzania inawathamini watanzania wote na inajivunia kuwa sehemu ya
makampuni ambao yameidhamini timu hiyo ili ikaiwakilishe nchi katika
mashindano ya mashua.
“NMB
ni benki ambayo inaongoza Tanzania na ipo kwa ajili ya watanzania, moja
ya sehemu ambayo tunaihudumia ni vijana, tunadhamini michezo mingi na
tunaamini ni sehemu nzuri kwa vijana wadogo maana wanatakiwa kuandaliwa
mapema,
“Mchezo
wa mashua una wachezaji wengi, NMB inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini
kwa vijana hawa ambao watawakilishi nchi, na tunaamini watarudi kutoka
Angola wakiwa na medali,” alisema Ineke.
Nae
Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari
aliishukuru NMB kwa msaada ambao imewapatia na kuelezea changamoto
mbalimbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo huo kutokana na kutokuwa
na wadhamini wanaowasimamia na kuwaomba NMB kuendeleza udhamini huo kwa
kipindi kirefu zaidi.
“Chama
chetu ndiyo kina dhamana ya kuongoza mchezo wa mashua nchini, mchezo
huu sio mgeni hata watu wanaovua ngalawa wanatumia mashua, mchezo wetu
unadumaa kwasababu hatuna udhamini na kama mnavyojua mchezo huu
unachezwa sehemu ya wazi kwahiyo hakuna anayelipa pesa, muda wote niwa
kujitolea,
“Mchezo
huu kwa sasa nchini unakuwa kama unashuka, tulianza kushiriki na watoto
12 lakini kwa sasa tunakwenda na watoto watano, mwanzo mgumu lakini
sisi tunaongeza juhudi na tunawashukuru NMB kwa hili wamelolifanya,”
alisema Nassari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni