Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemchangia
vifaa vya ujenzi Mjane Agripina Angelo Mkazi wa Kitoma Wilayani Karagwe
Mkoani Kagera.
Akimkabidi
vifaa hivyo kwa niaba ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali
(Mst) Salum Kijuu alisema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya hivyo baada
ya kuona kupitia vyombo vya habari jitihada za Mjane huyo kuanza
kuijenga nyumba yake upya kutokana na kuharibika baada ya tetemeko la
ardhi lililotokea mkoani humo mapema mwezi septemba.
Aidha
Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa wananchi ambao hawajaanza juhudi za
kurejesha makazi yao waige mfano wa mjane huyo kwa kuanza ujenzi wa
nyumba zao.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Bi. Agripina alisema kuwa anamshukuru
Rais kwa mchango huo kwani vifaa hivyo vitamsaidia kukamilisha ujenzi wa
nyumba yake na hatimaye kupata mahali pa kuishi yeye na familia yake
baada ya nyumba yake ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi.
Vifaa
alivyokabidhiwa mjane huyo ni pamoja na Mbao pisi 30, Mabati 35 ya futi
kumi ,Saruji mifuko 25 ,Misumari ya mabati kilo 4, Misumari ya kenchi
kg 7 na waya za kufungia makenchi kilo 3.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni