Hatimaye
Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo Cha Diplomasia.
Balozi
Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli
atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo
hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake
ikajazwa na Balozi John Kijazi, .
Aidha,
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine
Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia.
Wajumbe
hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed
Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni