Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Haya hapa Makusanyo ya Kodi mwezi Septemba 2016 chini ya Mamlaka ya Mapato (TRA):

Mkurugenzi wa Elimu na huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Bw. Richard Kayombo amesema mwenendo wa ukusanyaji mapato ya Serikali kwa sasa ni wa kuridhisha katika  kufikia  lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trioni 15.1 kwa mwaka fedha wa 2016/2017.

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekusanya Mapato ya shilingi trilioni 1.37 kwa Mwezi September kati ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.4 mwezi huo

Kuhusu zoezi la uboreshaji wa taarifa ya namba za utambulisho wa mlipa kodi linaloendelea jijini Dar es Salaam, Bw. Richard Kayombo amesema mpaka sasa TRA imetoa vyeti vipya vya TIN  kwa watu 15, 467 na zimebaki siku tisa kukamilisha zoezi hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni