Chama cha Tennis duniani ITF
kimempunguzia mchezaji nyota wa tennis Maria Sharapova adhabu ya kufungo
cha miaka miwili na sasa itakuwa miezi 15.
Katika taarifa yake chama hicho kimesema kuwa hakitakuwa tayari kupokea maelezo yoyote ambayo yanaonyesha kuwa mchezaji alitumia dawa hizo kwa maksudi baada ya taarifa zote kutolewa.
Sharapova ni mshindi mara tano wa Grand slam na kwa mujibu wa jarida la Forbes ni mwanadada anayelipwa zaidi katika mchezo huo kwa miaka 11 mfululizo mpaka alipopitwa na Serena Williams mwaka huu.
Sharapova aligundulika kutumia dawa hizo karibia mwezi mmoja tokea zilipofungiwa januari 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni