Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Mkuu wa Wilaya ya Chemba akemea wananchi kuua wenzao bila hatia.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Chemba ameyasema hayo leo wakati wakiaga mwili wa Mke wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kelema Balai aliyeuwa kwa kupigwa mshale wa sumu kijana ambaye mpaka sasa amekimbia na kutoweka hapo kijijini kutokana na ugomvi ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya mume wa marehemu na kijana anayehisiwa kutenda unyama huu.
Kijana anayehisiwa akiwa na wenzake wawili siku ya tukio majira ya saa mbili na nusu usiku walivamia nyumbani kwa marehemu na kuanza kumshambulia kwa fimbo mume wa marehemu na kukimbizwa hospital ya jirani kabla muhisiwa hajarejea na kutekeleza unyama huo.
Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi ambao ni baba wa kijana huyo kwa kuwa alishiriki katika tukio la awali la kumjeruhi Mwl Manyama kwa kushirikiana na kijana wake kumjeruhi kwa fimbo. (Mwl Manyama ndiye mume wa marehemu)
Watu wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji. Hawa wanashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya baada ya maelezo yao waliyoyatoa kuhusiana na namna walivyoshughulikia tukio hili kuanzia usiku mpaka asubuhi kuto mridhisha Mkuu wa Wilaya. Kwani toka usiku wa tarehe 3 mpaka saa tatu wahisiwa walikuwepo kijijini kabla ya kutoweka na Viongozi hao hwakuwa wamechukua hatua zozote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni