Rais
Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake
kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika
kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.
Rais
Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika
matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.
Wakati
wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza
changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo linalowakabili ni la
umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa
kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu
kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.
Aliposimama
kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO
mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli
akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga
na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si
hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.
Rais
Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake,
kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki
umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza
kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania,
kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.
Rais
Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha
umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.
Kuhusu
ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia gesi asilia inayopita jirani
na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni
Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza
kulishughulikia hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni