Baadhi ya wakazi wa halmashauri ya
mji wa bunda wamelalamikia serikali ya wilaya hiyo juu ya kukosekana kwa vivuko
vya waenda kwa miguu katika barabara
inayotoka mwanza kuelekea mjini musoma
,haswa katika maeneo ya bank ya NMB na Posta
mjini bunda.
Wakizungumza na Sauti ya Bunda kwa nyakati tofauti wakazi hao akiwemo James kibisa ,Naomi
kimarata na Emmanuely Thomas walisema
kuwa ni vema mamlaka husika ambao ni wakala wa barabara TANROADS wilayani
bunda, kuliangalia suala hilo kwani watembea kwa miguu wamekuwa wakipata wakati mgumu pindi
wanahitaji kuvuka katika barabara hiyo wakati wa jioni.
“Kiukweli siku hizi ni
shida hapa ukiwa unataka kuvuka katika maeneo haya ya posta na maeneo ya Bank
ya NMB haswa jioni” waliesema
Walisema ukosefu wa Alama hizo za
watembea kwa miguu imekuwa chanzo cha wengine kugongwa na magari ,pikipiki
ambapo walitumia nafasi hiyo kuiomba serikali ya halmashauri ya mji wa bunda kutatua
kero hiyo kwani imekuwa kero kwa muda sasa.
Hata hivyo, Sauti ya bunda Blog inaendelea
kuwatafuta wahusika ambao ni tanroads ili kuweza kuweka bayana juu ya
suala hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni