Mgombea urais mwenza wa chama cha
Republican nchini Marekani Mike Pence na mwenzake wa Democratic Tim
Kaine wamelumbana kuhusu taarifa za kodi za Donald Trump kwenye mdahalo
wa runinga.
Bw Pence, ambaye ni gavana wa Indiana, amesema mgombea urais wa chama cha Republican Bw Trump alitumia "werevu" katika kutumia sheria za kodi kukwepa kulipa kodi.
Lakini Bw Kaine, seneta wa Virginia, alipinga wazo hilo la "werevu" akishangaa iwapo ilikuwa busara kukwepa kulipa pesa za kutumiwa kulipa wanajeshi au kufadhili elimu shuleni.
Bw Trump ameshutumiwa sana kutokana na rekodi yake ya ulipaji kodi.
Amekataa kufichua taarifa zake za ulipaji kodi lakini gazeti la New York Times majuzi lilifichua kwamba huenda amekwepa kulipa kodi kwa miaka 18 iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni