Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Wakazi wa Bunda waomba wawekewe alama za watembea kwa miguu katika Barabara ya Musoma > Mwanza



Baadhi ya wakazi wa halmashauri ya mji wa bunda wamelalamikia serikali ya wilaya hiyo juu ya kukosekana kwa vivuko vya waenda kwa miguu katika barabara  inayotoka  mwanza kuelekea mjini musoma ,haswa katika maeneo ya bank ya NMB  na Posta mjini bunda.

Wakizungumza na  Sauti ya Bunda kwa nyakati tofauti wakazi hao akiwemo James kibisa ,Naomi kimarata na Emmanuely Thomas  walisema kuwa ni vema mamlaka husika ambao ni wakala wa barabara TANROADS wilayani bunda, kuliangalia suala hilo kwani watembea  kwa miguu wamekuwa wakipata wakati mgumu pindi wanahitaji kuvuka katika barabara hiyo wakati wa jioni.

“Kiukweli siku hizi ni shida hapa ukiwa unataka kuvuka katika maeneo haya ya posta na maeneo ya Bank ya NMB haswa jioni” waliesema

Walisema ukosefu wa Alama hizo za watembea kwa miguu imekuwa chanzo cha wengine kugongwa na magari ,pikipiki ambapo walitumia nafasi hiyo kuiomba serikali ya halmashauri ya mji wa bunda kutatua kero hiyo kwani imekuwa kero kwa muda sasa.

Hata hivyo, Sauti ya bunda Blog  inaendelea  kuwatafuta wahusika ambao ni tanroads ili kuweza kuweka bayana juu ya suala hilo.


Agizo la Rais Magufuli kwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi nyingine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 07 Oktoba, 2016 amekutana na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani ambapo pamoja na mambo mengine ametaka utekelezaji wa diplomasia ya uchumi utiliwe mkazo katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

Katika Mkutano huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Magufuli aliyehutubia na kuongoza majadiliano juu ya masuala mbalimbali ya shughuli za mabalozi, alisema Tanzania imeweka dhamira ya kuikuza sekta ya viwanda kutoka ukuaji wa asilimia 7.3 hadi kufikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2021 na kuzalisha ajira kwa asilimia 40.

“Sasa nimeona niwaite waheshimiwa Mabalozi ili tuelewane, mjue mwelekeo tunaoutaka na mjue ni namna gani mtakavyoshiriki kuhamasisha uwekezaji wa viwanda.

“Nataka badala ya kubaki mmejifungia ofisini, mtoke mwende mkawatafute wawekezaji waje wawekeze katika viwanda ili nchi yetu inufaike kwa watu wetu kupata ajira, Serikali kukusanya kodi na tuinue maendeleo yetu” alisema Rais Magufuli.

Maeneo mengine ambayo Rais Magufuli ametaka Mabalozi wayafanyie kazi ni kutangaza na kuwavutia watalii kuja hapa nchini, kufanyia kazi fursa zote zenye manufaa kwa Tanzania katika nchi wanakowakilisha, kulinda mali za nchi zilizopo katika nchi hizo na kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya biashara na uwekezaji inayofanywa kati ya Tanzania na nchi wanakowakilisha.

Pia Rais Magufuli aliwataka waheshimiwa Mabalozi wote kufanya kazi kwa juhudi, kuondoa kasoro za utendaji kazi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa katika ofisi zao na kubana matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima.

Dkt. Magufuli aliitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujipanga na kudhibiti mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zimekuwa zikitumika katika safari za nje ya nchi na matumizi mengine yasiyo ya lazima, pamoja na kuhakikisha watumishi wote ambao wapo katika ofisi za ubalozi kwenye nchi mbalimbali bila sababu za msingi wanarejeshwa nchini ili kupunguza mzigo wa gharama kwa Serikali.

“Kuna wafanyakazi wapo kwenye Balozi zetu wakati hata sifa za kuwa katika nafasi wanazoshikilia hawana, ilifika mahali mtu akiharibu hapa nyumbani anapangiwa ubalozini.

“Wakati mwingine unakuta ubalozi wa Tanzania kwenye nchi fulani una idadi kubwa ya wafanyakazi kuliko mahitaji ya ubalozi huo, haiwezekani” alisisitiza Rais Magufuli.

Hata hivyo Dkt. Magufuli aliwapongeza Mabalozi wote wa Tanzania kwa kazi wanazozifanya kwenye nchi wanazowakilisha na amewahakikishia kuwa Serikali ina matumaini nao na inawategemea kuwa wataendelea kuiwakilisha na kuitangaza vizuri Tanzania.

Mkutano huo pia ulihuduriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa Taasisi mbalimbali na Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Daktari asema haya juu Kijana Said Ally Aliyetobolewa Macho Na Scorpion.

MAJONZI na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati Kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion Buguruni Sheli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam jana asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia kujeruhiwa vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza uwezekano wa kuona.
"Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui mungu anampango gani na mimi wala sijui nini  hatima ya maisha yangu" alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari  na simanzi huku mke wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.

Mrisho alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata matibabu lakini imeshindikana kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo hataweza kuona tena katika maisha yake.
 
"Kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa" alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema wamepokea kwa huzuni taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.
 
Makonda alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze  kumsaidia wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu wengine kwa ajili ya kumsaidia.

Makonda alisema serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa atakuwa haoni.

"Pamoja na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo" alisema Makonda.

Walimu Wanafunzi Waliompiga Mwanafunzi Mbeya wasitishiwa Mikopo na Bodi ya Mikopo



Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo.

1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)

4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)

Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwa hiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo. 
Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.

Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.

Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji

Ijumaa, Oktoba 7, 2016

Redio Mazingira fm wamwangiwa sifa kwa utendaji wao wa kazi.



Diwani wa kata ya Bunda Mjini katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoa Mara Joash Kunaga ameipongeza Redio Mazingira Fm (sauti ya jamii) iliyopo mjini Bunda kwa kazi kubwa  wanayoifanya ya kuhabarisha jamii kupitia vipindi vyao vya kila siku hali ambayo imesaidia pa kubwa katika jamii kufahamu mengi.

Joash aliyazungumza hayo wakati alipotembelea studi za redio hiyo zilizopo mtaa wa Bank ya NMB mjini ambapo alisema hana budi kuishukuru redio hiyo kwa kuelimisha jamii juu ya maswala mbalimbali ya kijamii.
“ni siwe mchoyo wa sifa kiukweli niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya kwani inaonyesha matokeo chanya kwa jamii” alisema

Katika hatua nyingine Diwani huyo aliwataka viongozi pamoja na wafanyakazi wa redio hiyo waendelee kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuendelea kuwa vizuri katika uhabarishaji.

faida za tendo kwa wachezaji wa mpira




Mara kadhaa tumesikia wachezaji wakisakamwa na baadhi ya viongozi wakati mwingine mashabiki wao kwamba wanafanya mapenzi mara kwa mara kitu ambacho kinapelekea kuporomoka kwa viwango vyao kiuchezaji wawapo uwanjani.
Ili kupata uthibitisho wa kisayansi, kama kuna uhusiano wowote wa mchezaji kufanya mapenzi mara kwa mara na kudorora kwa kiwango chake, Dkt. Yomba ametoa ufafanuzi kuhusiana na wachezaji na ufanyaji mapenzi mara kwa mara, kuna faida au hasara gani kwa mchezaji kushiriki tendo hilo.
“Kimsingi inaweza ikaleta athari au isilete athari ikawa ni faida, inapokuwa zaidi inaweza ikaleta, madhara lakini inapokuwa kidogo inakuwa na faida mara mbili,” anathibitisha Dkt. Yomba kwa kusema inategemea na mtu atafanya mapenzi kwa kiwango gani.
“Katika mwili wa binadamu kuna kitu kinaitwa hormone, hii ni aina ya vimeng’enywa ambavyo vinakuwepo mwilini, vinasababisha vichocheo katika kazi mbalimbali mwilini. Kuna kitu kinaitwa testosterone , hiki ni kimeng’enyo kwa mwanaume mara nyingi kinapatikana kwenye ‘kende’ zake, kwa mwanamke kinapatikana kwenye mayai (ovaries) lakini kwa kidogo sana huwa kinapatikana kwenye figo.”
“Kinazalishwa kwa wingi kisha kinaingia kwenye damu ambapo inakuwa rahisi kwacho kuzunguka mwilini, kwahiyo hiki kimeng’enyo kinapozaliwa kinapita mpaka kwenye upongo kupitia damu, kinaboreshwa na kina kazi nyingi sana kwa mwanaume na mwanamke, lakini kazi moja wapo ni kujenga misuli yaani kinaimarisha misuli na kufanya mifupa kuwa imara.”
“Kwahiyo kama testosterone ikiwa nyingi kazi yake kubwa ni kusaidia kujenga misuli na kuimarisha mifupa, kwa mchezaji akiwa na vitu hivi viwili basi inamaana vitamsaidia anapokuwa uwanjani kama misuli yake inakuwa imejengeka na mifupa yake inakuwa imara basi inamsaidia.
“Kwanini nimeanza kwanza kuielezea hii hormone, nimeielezea kwasababu wanasayansi wanasema, kufanya mapenzi (tendo la ndoa) ina-boost hiyo hormone kuzalishwa kwa wingi. Kwa maana hiyo ikiwa inazaliwa kwa wingi, inaenda kuleta uimara wa nyama na misuli pamoja na kuipa nguvu miguu.”
“Kwa kuangalia kazi hiyo, kwamba inapozaliwa kwa wingi inaenda kuimarisha misuli, basi inaleta maana kwa mchezaji kwamba kama atashiriki mapenzi kwa sababu hiyo, inaweza ikamuimarisha kwa kumpa nguvu katika misuli yake na kuimarisha miguu. Kwahiyo hapo tunaiona faida kwasababu nimeshaeleza umuhimu wake na kazi yake kubwa mwilini ni nini.”
“Hizi faida utazipata vizuri zaidi kwa kupata nafasi ya kushiriki kwa mtu wako kama ni mkeo au mpenzi wako na unatakiwa kuamini kabisa kufanya mapenzi kabla ya mechi haiwezi kuathiri performance, badala yake uta-perform zaidi.”
Mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima aliwahi kuweka wazi kwamba, yeye hupenda kufanya tendo la ndoa kabla ya mechi hususan mechi kubwa akisema huwa inamfanya kuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya timu anayokutana nayo.