Jumamosi, 28 Mei 2016

Korea Kaskazini yaonya meli za Korea Kusini




Korea Kaskazini inasema itashambulia meli yoyote kutoka Korea Kusini, itakayovuka mpaka wa baharini kati ya mataifa hayo mawili unaozozaniwa.

Onyo hilo linajiri baada ya Korea Kusini kushambulia meli mbili za Korea Kaskazini zilizovuka mpaka wake kwa muda mfupi.

Pyongyang imetaja shambulizi hilo kama uchokozi wa kijeshi, lengo likiwa kusababisha hali ya wasiwasi.

Mapema mwezi huu ,Korea Kusini ilikataa wito wa Korea Kaskazini,ikisema kwamba lazima Pyongyang ichukue hatua kusitisha mpango wake wa nuklia kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni